SEKTA BINAFSI YASHIRIKI UKUSANYAJI MAONI YA KODI KIGOMA

Serikali inakusanya maoni ili kuboresha Sera ya uutozaji kodi kwa mwaka 2024/25 kwa kuhusisha makundi mbalimbali kwenye Sekretarieti ikiwemo Sekta binafsi ili kuwa na Sera madhubuti yenye kukidhi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya wadau wa kodi nchini. Hayo yameelezwa na Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, wakati wa Kongamano la ukusanyaji maoni ya Kodi Kikanda mkoani Kigoma, ikiwa ni muendelezo wa makongamano kama hayo yanayofanyika Kanda mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha Sera ya Kodi kwa mwaka 2024/25.