RAIS SAMIA KUZINDUA SERA YA TAIFA YA USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI JIJINI DODOMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya Mwaka 2025, tarehe 08 Aprili 2026 katika Ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre uliopo jijini Dodoma. Hayo yalibainishwa na Kaimu Kamishna Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bw. Alex Haraba, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.