RAIS DKT SAMIA AUPONGEZA UONGOZI WA WILAYA YA KIGAMBONI KWA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA VITENDO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam, Bi. Halima Bulembo na viongozi wenzake kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili jamii katika Wilaya hiyo kwa vitendo.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi hizo leo alipompigia simu Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akihutubia Wakazi wa Kigamboni katika eneo la Mji Mwema, akimwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, katika hafla ya kupokea na kukabidhi vifaa mbalimbali kwa makundi maalum katika Wilaya ya Kigamboni.