NORWAY KUKIJENGEA UWEZO KITUO CHA UBIA KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI

Norway imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika kukijengea uwezo Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kuiwezesha sekta binafsi kushiriki kikamilifu kujenga Uchumi wa nchi. Hayo yameelezwa jijini Dodoma, na Mhe. Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes, kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.