NCHI ZA AFRIKA ZAKUBALIANA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUONGEZA MAPATO

Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi wa nchi za Afrika wamekubaliana kuhakikisha wanakusanya na kutumia rasilimali zilizopo vizuri pamoja na kuboresha matumizi ya teknolojia ili kuongeza ukusanyaji wa mapato. Hayo yamesemwa Mjini Victoria Falls, Zimbabwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 56 wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi kutoka Afrika unaoratibiwa na Kamisheni ya Uchumi wa Afrika chini ya Umoja wa Mataifa (UNECA)