NCHI ZA AFRIKA ZAJADILI KUKUZA MAPATO YA NDANI KUEPUKA UTEGEMEZI WA MISAADA NA MIKOPO KUTOKA NJE

Nchi 14 za Afrika za Sub-Sahara za Kundi la Kwanza ambazo ni wanachama wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), zimekubaliana kuimarisha mikakati ya kukuza uwekezaji kutoka sekta binafsi na kuimarifa mifumo ya makusanyo ya mapato ya ndani katika nchi zao ili kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa fursa za mikopo na misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo. Hayo yameelezwa wakati wa Mkutano wa 52 wa Kundi la Kwanza la nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency Policy Dialogue), uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.