NAIBU KATIBU MKUU, ELIJAH MWANDUMBYA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya ametembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amepongeza mikakati iliyowekwa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Wizara na Taasisi zake.
Bw. Mwandumbya alisema kuwa Wizara ya Fedha ni Wizara muhimu katika kuchochea maendeleo ya mchi hivyo ni muhimu elimu ikatolewa kwa usahihi na ufanisi ili watanzania waweze kuelewa majukumu ya Wizara na Taasisi zake.