MWANDUMBYA: TUTAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na uwekezaji na kuitaka iendelee kutekeleza wajibu huo wenye tija. Ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati wa Mahafali ya 18 ya Chuo cha Kodi cha TRA yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana.