MWANDUMBYA ATOA RAI KWA MAAFISA MASUULI KUBORESHA UKUSANYAJI MAPATO YASIYO YA KODI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya ametoa rai kwa Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kuendelea kutekeleza majukumu yao ya ukusanyaji wa mapato kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo suala la uwasilishaji wa mapato ya Serikali katika Mfuko Mkuu wa Serikali kwa wakati.
Bw. Mwandumbya ametoa rai hiyo wakati wa kufunga Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.