MKUU WA MKOA ARUSHA ATEMBELEA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela (katikati), akiwasili katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha yanapofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akielezea kuhusu mpangilio wa washiriki katika maadhimisho hayo.