MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA MAENDELEO TIB ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania - TIB, Bi. Lilian Mbassy, ametembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amezipongeza Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu sera za uchumi na fedha, program, huduma, uwekezaji, benki na masuala mengine kwa umahiri.