MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII INAONDOA UTEGEMEZI UZEENI

Wananchi wanatakiwa kupata elimu ya fedha na kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuwasaidia wanapozeeka au kustaafu kazi ili kuondoa utegemezi. Wito huo umetolewa mkoani Morogoro na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Fedha kwa Wasanii kutoka Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji wa Elimu ya Uraia (TACCI) wanaolengwa kupeleka elimu ya fedha vijijini.