MHE. RAIS DKT. MWINYI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA FEDHA BALOZI OMAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar, leo tarehe 18 Februari, 2026. Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Omar, aliambatana na Manaibu Waziri wake Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) na Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), pia Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Khamis Shaaban.