MHE.MWIGULU AWATAKA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KUSAIDIA KUKUZA SEKTA BINAFSI NCHINI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameiagiza Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA), kusaidia kukuza Sekta Binafsi nchini ambayo itasaidia kuongeza kipato, kukuza uchumi wa nchi na itatoa fursa kwa vijana wengi kujiajiri. Mhe. Dkt. Nchemba alitoa maagizo hayo wakati akiongea na wananchi wa Kilambo, Kata ya Njisi Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya, mara baada ya kufanya ziara yake ya kukagua shughuli za kiuchumi na maendeleo katika Kituo cha Forodha cha Pamoja-Kasumulu kilichopo mpakani mwa Tanzania na Malawi.