MHE. MUNDE AHIMIZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MADINI YA GRAPHITE MOROGORO
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amehimiza utekelezaji wa Mradi wa uchimbaji madini ya Graphite uliopo Mahenge Mkoa wa Morogoro ili uanze kutoa manufaa yaliyotarajiwa kwa watanzania kwa wakati.
Rai hiyo imetolewa Ofisini kwake jijini Dodoma wakati wa mkutano kati yake na Ujumbe wa Kampuni ya Faru Graphite Corporation Limited ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Paul Sims.
