MHE. MUNDE AAGIZA HAZINA SACCOS KUIMARISHA USIMAMIZI WA FEDHA ZA WANACHAMA.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) ameiagiza Menejiment ya Hazina Saccos kuhakikisha fedha za wanachama zinalindwa kwa kiwango cha juu, huku akiwataka kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji, ukaguzi wa ndani na udhibiti wa mikopo pamoja na urejeshaji wake. Mhe. Munde aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Hazina Saccos Ltd uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Morena, Mjini Morogoro.