MHE. LUSWETULA: VIJANA TUMIENI MITANDAO YA KIJAMII KUBUNI FURSA ZA KUJIKWAMUA KIUCHUMI.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Degratius Luswetula (Mb), amerejea wito wake kwa vijana kutumia teknolojia hususani Akili Mnemba (AI) na mitandao ya kijamii ili kubuni fursa za kiuchumi na kuongeza kipato. Mhe. Luswetula amesema hayo wakati wa Mahafali ya 23 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) -Kampasi ya Dar es Salaam, Zanzibar na Tanga yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho, Kurasini jijini Dar es Salaam.