MHE BALOZI OMAR: TANZANIA NA SINGAPORE KUKUZA ZAIDI USHIRIKIANO WA KIUCHUMI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema Tanzania iko tayari kushirikiana zaidi na Singapore katika sekta za kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo kukuza biashara na uwekezaji, utalii, matumizi ya akili unde (Artificial Intelligence) pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato ya Serikali kwa njia ya kidigitali. Mhe. Balozi Omar ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Singapore nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Singapore, Mhe. Douglas Foo, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kidiplomasia.