MHE BALOZI OMAR KUSHIRIKI MKUTANO WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA NCHINI CONGO BRAZAVILLE.
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewasili nchini Congo, Brazzaville, amabako atashiriki Mkutano Mkuu wa 61 wa mwaka 2026 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 mwaka 2026, katika Mji Mkuu wa Congo, Brazaville.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Brazaville, Maya Maya, Mheshimiwa Balozi Omar, alilakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Congo, Brazaville, Mhe. Said Juma Mshana.
Katika msafara huo, Mhe. Balozi Omar, ambaye ni Gavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali ambaye pia katika Muundo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni Gavana Mbadala wa Benki hiyo (Alternative Governor), Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Kamishna wa Fedha za Nje, Bw. Rished Bade.
