MHE. BALOZI OMAR AWATAKA WAHITIMU WA TIA ZANZIBAR KUWA WATATUZI WA CHANGAMOTO KUELEKEA DIRA 2050
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewataka wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Zanzibar kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya umma na binafsi nchini kupitia taaluma waliyoipata.
Akizungumza katika Mahafali ya kwanza ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Zanzibar, Mhe. Balozi Omar alisisitiza kuwa wahitimu hao wanapaswa kuwa suluhu ya kweli katika utekelezaji wa Dira 2050 huku akibainisha kuwa sekta binafsi ina kazi kubwa ya kutekeleza asilimia 70 ya Dira hiyo.
