MHE. BALOZI OMAR AWASILI BANGKOK KUSHIRIKI MIKUTANO YA MWAKA YA IMF NA BENKI YA DUNIA.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewasili jijini Bangkok nchini Thailand, ambapo ataongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), inayofanyika nchini humo kuanzia tarehe 12 hadi 18 Oktoba 2026.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Suvarnabhumi, Mhe. Balozi Omar, aliyeambatana na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, alilakiwa na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Thailand, Mhe. Florean Rwehumbiza pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni Kaimu Mshauri Mkuu wa Usimamizi na Uendelezaji wa Ukusanyaji wa Mapato wa Thailand, Bw. Yutuna Phoolpipat.
