MHE. BALOZI OMAR AKAGUA JENGO JIPYA LA KISASA LA OFISI YA WIZARA YA FEDHA
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Jengo jipya la kisasa la Ofisi za Wizara ya Fedha lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma, litawawezesha watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi katika mazingira bora na kuwahudumia wananchi na wadau wake wengine kwa ufanisi zaidi.
Mhe. Balozi Omar, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo hilo akiambatana na Naibu Mawaziri wake wawili, Mhe. Larent Luswetula, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, na Menejimenti ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.
