MHE. BALOZI OMAR AKABIDHI TUZO ZA UBUNIFU ZA TRA
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekabidhi tuzo za fedha taslim, ngao na vyeti kwa washindi 9 waliowasilisha mawazo bora ya ubunifu yatayosaidia katika kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Serikali na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zenye thamani ya shilingi milioni 240, zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, baada ya kushindanisha mawazo bunifu 5,681 yaliyowasilishwa na wananchi pamoja na watumishi wa TRA, kuanzia mwezi Mei, 2025.
Mawazo Bunifu hayo yanahusisha ubunifu wa Mifumo ya Tehama ambayo imebuniwa na vijana wa kitanzania inayotarajiwa kutumiwa na TRA kuboresha wigo wa walipa kodi, kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiforodha na ulipaji kodi kwa njia rahisi na yenye ufanisi kutoka kwa walipakodi.
