MHE. BALOZI OMAR AISHAURI EADB KUCHOCHEA ZAIDI UKUAJI WA MAENDELEO KANDA YA AFRIKA MASHARIKI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar ameishauri Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) kuongeza ubunifu katika kushirikiana na Serikali pamoja na Sekta binafsi ili kuchangia katika maendeleo ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ametoa ushauri huo jijini Dodoma alipokutana na kuzungumza na uongozi wa benki hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na fursa za ushirikiano kati ya Serikali na benki hiyo, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square.