MHE. BALOZI OMAR AIPONGEZA NA KUIHIMIZA YAS TANZANIA KUWEKEZA ZAIDI KUENDANA NA MALENGO YA DIRA 2050

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameipongeza Kampuni ya Mawasiliano ya YAS Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika kukuza sekta ya mawasiliano nchini na kuitaka iongeze uwekezaji katika miundombinu na huduma za mawasiliano ya kidijitali ili kuendana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Mhe. Omar ametoa pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya YAS Tanzania katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala ya uwekezaji na nafasi ya sekta ya mawasiliano katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya teknolojia nchini.