MHE. BALOZI OMAR: AIMWAGIA SIFA TRA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameimwagia sifa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA kwa utendaji uliotukuka uliowezesha Mamlaka hiyo kuendelea kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kila mwezi na kueleza imani yake kwamba kwa kushirikiana na alipakodi, wataweza kuvuka lengo walilopangiwa la kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 42 katika Mwaka wa Fedha 2026/2027.
Mhe. Balozi Omar, ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya TRA, Kizimkazi, Zanzibar, litakalokuwa na ghorofa moja, ambapo hadi kukamilika kwake linatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.6.
