MFUMO WA HAZINA MACHAPISHO KIMBILIO KWA WATAFITI WA UCHUMI

Msimamizi wa Kitengo cha Maktaba, Wizara ya Fedha, Bi. Pendo Kavalambi, amesema kuwa Mfumo wa Hazina ya Machapisho (Mof respository) umekuwa nyenzo muhimu kwa wananchi wakiwemo wanaofanya tafitini kuhusu masuala ya uchumi na fedha. Amesema hayo jijini Dodoma wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.