MAWAZIRI WA FEDHA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA ARUSHA KUJADILI KODI NA USHURU

Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wamekubaliana kuandaa orodha ya bidhaa zitakazohusika na uondoaji wa kodi na ushuru mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa itifaki ya ushirikiano ili kuchochea biashara na uwekezaji katika Jumuiya hiyo. Makubaliano hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambaye ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha.