MATUKIO WAKATI WA MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DODOMA

Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Bi. Fauzia Nombo (mbele) akiwaongoza baadhi ya watumishi wanawake wa wizara ya Fedha kwa niaba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El-maamry Mwamba, waliojitokeza katika maandamano kusherehekea kilele cha Siku ya Wanawake yaliyofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali II, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma.