MAONI YA MABORESHO SERA YA KODI KURAHISISHA ULIPAJI KODI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amewataka wafanyabiashara kutoa maoni ya uboreshaji wa Sera za Kodi kupitia Timu ya wataalamu wa Uchambuzi wa Sera za Kodi kutoka Wizara ya Fedha ili waweze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Rai hiyo imetolewa Mkoani Shinyanga wakati wa Kongamano la Jukwaa la Wafanyabiashara lililoandaliwa na Mkoa huo ambalo lilitumika kukusanya maoni ya Uboreshaji wa Sera ya Kodi kwa mwaka wa Fedha 2024/25 Dkt. Abdallah, alisema kuwa eneo muhimu katika ufanyaji biashara ni Kodi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anawataka watu walipe kodi lakini Mamlaka za kukusanya kodi zikusanye kodi kwa weledi bila kuleta mgongano.