MAFUNZO YA WARATIBU HUDUMA NDOGO ZA FEDHA YAHITIMISHWA

Waratibu wa huduma ndogo za fedha nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ili kuboresha huduma za fedha na kuleta maendeleo ya kiuchumi hapa nchini. Hayo yalisemwa na Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa waratibu wa Biashara ya Huduma ndogo za Fedha na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika ngazi ya Wizara, Mikoa na Halmashauri, jijini Dodoma.