MAAFISA MASUULI WAASWA KUSIMAMIA MALI ZA SERIKALI KIKAMILIFU
Serikali imewasisitiza Maafisa Masuuli nchini kuzingatia misingi ya uwajibikaji, ufanisi na uwazi katika kuhakikisha kwamba, mali za umma zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote.
Rai hiyo imetolewa Jijini Arusha na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya usimamizi wa Mali za Serikali wa Wizara ya Fedha, Bw. Ismael Ogaga, wakati akifungua Mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma kwa Maafisa Masuuli, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo.