MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA YAANZA RASMI JIJINI TANGA

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwa mwaka 2026 yameanza rasmi leo tarehe 19 Januari, 2026 katika Viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya fedha, ikiwemo matumizi sahihi ya huduma za kifedha, umuhimu wa kujiunga na mifumo rasmi ya fedha pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiuchumi kwa maendeleo endelevu.