LUSWETULA: SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA UFANYAJI BIASHARA NCHINI

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), ameihakikishia jumuiya ya wafanya biashara na wajasiriamali nchini kwamba Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kukuza biashara zao. Mhe. Luswetula ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na jumuiya ya wafanyabiashara mjini Mpanda mkoani Katavi ambapo amesisitiza kuwa hatua hiyo imelenga kuongeza tija katika biashara na mapato ya Serikali kwa ujumla Kupitia ulipaji kodi.