KOICA KUONGEZA NGUVU UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, amesema Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA), kupitia mpango uliotiwa saini mwaka 2014 limetoa ruzuku ya jumla ya Dola za Kimarekani milioni 139.5 sawa na Sh. bilioni 356.3 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Dkt. Mwamba alibainisha hayo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea anayeshughulikia mambo ya kimkakati (KOICA) Don Ho Kim, aliye katika ziara ya kikazi Tanzania.