KODI KUFANYIWA MAREKEBISHO KILA BAADA YA MIAKA MITATU
Serikali imeeleza kuwa itakuwa inafanya marekebisho ya kodi kila baada ya miaka mitatu ili kuwa na Sera ya kodi inayotabirika na kuwafanya wawekezaji kuweka mipango yenye ufanisi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, wakati wa Kongamano la ukusanyaji maoni ya Kodi Kikanda Jijini Mbeya, ikiwa ni mwendelezo wa makongamano kama hayo yanayofanyika Kanda mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha Sera ya Kodi kwa mwaka 2024/25.