KAMATI YA BUNGE BAJETI YAIDHINISHA MAKADIRIO MWAKA WA FEDHA 2024/2025

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeidhinisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya mafungu nane (8) ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Jijini Dodoma, ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Sillo (Mb), amemkabidhi Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), maelekezo ya maeneo maalum ya kuzingatia ili kuboresha mpango na bajeti ya Wizara.