KAFULILA AELEZEA MKAKATI WA KUVUTIA TRILIONI 21 ZA PPP
Serikali inapanga kukutanisha wakuu wa mashirika ya umma 7 ya kimkakati na wabobezi wa uwekezaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) mwezi ujao kwa lengo la kubadilishana uzoefu utakaosaidia kuvutia mitaji ya kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 9 (sawa na Sh. trilioni 21) ndani ya miaka mitatu.
Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila. alisema kuwa mkutano huo utakaofanyika Mei 2-6 ni sehemu ya mkakati wa kufikia malengo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDPIII).