JAPAN YAONGEZA SH. BILIONI 8.9 UKARABATI WA BANDARI YA KIGOMA

Tanzania imepokea msaada wa nyongeza wa Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma baada ya marekebisho ya mikataba miwili ya msaada kati ya Tanzania, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Ubalozi wa Japan. Mikataba ya marekebisho ya msaada imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan Tanzania, Bw. Hitoshi Ara, kwa niaba ya Japan.