IMF NA EAC WAJADILI UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI KWA AJILI YA MAENDELEO

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza katika mkutano uliotishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Wadau kutoka nchi za Afrika, wakati wa mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings), jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo wadau walijadili namna nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinavyoweza kujitegemea kwa kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani badala ya kutemea mikopo na misaada kutoka nje.