ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WAKULIMA NA WAFUGAJI MLANGALI

Wakulima na wafugaji wa Kata ya Mlangali, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamepatiwa elimu ya usimamizi wa fedha kwa lengo la kuwawezesha kuongeza tija katika shughuli zao za uzalishaji, kuboresha kipato na kuimarisha ustawi wa kiuchumi. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Afya Mlangali, yametolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) pamoja na Dhamana ya Uwekezaji na Usimamizi Rasilimali Tanzania, (UTT AMIS).