EAC KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA VISIVYO VYA KIFORODHA

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs), huku vikwazo nane vikiendelea kushughulikiwa, na vikwazo vingine vipya vinne vimewasilishwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara baina ya nchi hizo. Vilevile, nchi hizo zimekubaliana kutoza kiwango cha dola 10 za kimarekani kwa kilomita 100 kwa ajili ya matumizi ya barabara (road user charge) kwa magari ya mizigo kutoka nchi moja kwenda nyingine katika Jumuiya hiyo badala ya kila nchi kuwa na viwango vyake vya tozo.