DKT. YONAZI AKOSHWA NA KOZI YA USALAMA WA MTANDAO VYUO VYA WIZARA YA FEDHA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, amevipongeza Vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Fedha kwa kuwa na programu zinazoendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia. Dkt. Yonazi, alitoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam ambapo Vyuo hivyo kikiwemo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanzisha Kozi ya Usalama Mtandaoni (Cyber Security)