DKT. NCHEMBA ATETA NA WAZIRI WA VIWANDA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya viwanda na Biashara ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake katika Uchumi na maendeleo ya watu. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.