DKT. NCHEMBA ATETA NA WAZIRI WA UJENZI

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya ujenzi ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake katika Uchumi na maendeleo ya watu. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.