DKT. NCHEMBA ATETA NA VIONGOZI WA WIZARA YA UJENZI NA TAMISEMI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati) akiongoza kikao kilichowashirikisha Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius Ndejembi, pamoja na Makatibu Wakuu na Viongozi waandamizi wa Wizara hizo tatu; TANROADS na TARURA, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya barabara, Ofisini kwake (Treasury Square), Jijini Dodoma.