DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA IMF KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameliambia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwamba utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali unaathiriwa na hali mbaya ya hewa inayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi ambapo kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi kinaelekezwa kukabiliana na athari za mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kufuatia mvua za el nino zinazoendelea kunyesha.