DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kupanua biashara zake hapa nchini na kuitaka Benki hiyo ishushe zaidi riba ili wananchi wakiwemo watumishi wa Umma waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na Benki hiyo. Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na Uongozi wa Benki hiyo Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo walijadili namna Benki na Serikali zinaweza kushirikiana kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi.