DKT NCHEMBA ATETA NA UJUMBE KUTOKA SHIRIKALA MAREKANI LA CHANGAMOTO ZA MILENIA-MCC

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameishukuru Marekani kupitia Shirika lake la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) kwa kuiteua Tanzania kuwa moja ya nchi zilizoko kwenye mpango wa kunufaika na ruzuku zinazolenga kusaidia mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kutatua vikwazo vya ukuaji uchumi. Dkt. Nchemba amesema hayo Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika hilo la Changamoto za Milenia-MCC, ukiongozwa na Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wake, Bi. Chidi Blyeden.