DKT NCHEMBA ATETA NA BALOZI WA DENMARK NCHINI TANZANIA-MEMA YAJA

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru Denmark kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida. Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mheshimiwa Mette Dissing-Spandet, Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo walijadili masuala kadhaa ya ushirikiano.